Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kulingana na vyanzo vya Kiebrania, ongezeko la bei za tiketi za ndege pamoja na kufutwa kwa safari za ndege za kimataifa kadhaa kuelekea viwanja vya ndege vya Israel, kumesababisha mdororo wa kiuchumi unaoendelea.
Kwa ufafanuzi zaidi, safari moja ya ndege ya kimataifa kutoka Israel kwenda Cyprus imeongezeka kutoka dola 210 hadi dola 267, huku bei ya tiketi za ndege kutoka nchi nyingine kwenda Israel ikiwa imeshuka kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, safari ya ndege kutoka Hungary kwenda Israel imeshuka kutoka dola 181 hadi dola 141. Ingawa hii ni punguzo la kipekee la bei, lakini linaashiria mdororo wa kiuchumi, kulingana na gazeti moja la Kiebrania.
Kulingana na takwimu za Ofisi ya Takwimu ya Ardhi Zilizokaliwa kwa Mabavu, Wazayuni kwa sasa wanatumia kiasi kikubwa zaidi cha pesa kwa ajili ya safari za ndege kuliko zamani.
Moja ya sababu za kudorora huku ni kufungwa kwa anga ya Israel na Yemen, jambo ambalo ni jibu kutokana na uvamizi, vita, mauaji na jinai zinazofanywa na Israel huko Ghaza. Hali hii imesababisha njia za ndege za Israel kutokuwa salama mbele ya jamii ya kimataifa.
Bila shaka, wahalifu wa serikali ya Netanyahu wamekubali kubeba dhamana ya kuzorota kwa hali ya usalama na kuongezeka kwa hofu miongoni mwa wahamiaji, hata katika nyumba zao wenyewe.
Maoni yako